1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL: Wito kuachilia huru mahabusu wa Korea ya Kusini

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgS

Rais wa Korea ya Kusini,Roh Moo Hyun ametoa wito wa kuwaachilia huru moja kwa moja wananchi wenzake 23,waliotekwa nyara siku ya Alkhamisi, nchini Afghanistan.Amesema,kwa hali yo yote ile kusitokee hasara ya maisha.Alipozungumza kwenye televisheni kulihotubia taifa,Rais Roh alisema, serikali yake ipo tayari kujadiliana na wahusika, ili raia wa Korea ya Kusini wapate kuachiliwa huru,upesi iwezekanavyo.