1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sera ya kigeni: Saudi Arabia yaigwaya Marekani

Admin.WagnerD3 Desemba 2013

Licha ya kuzinunia nchi za magharibi kutokana na nchi hizo kuisogelea tena Iran kidiplomasia, Saudi Arabia haina uwezekano mkubwa wa kuchagua kufuata siasa ya mambo ya nje inayoitaka.

https://p.dw.com/p/1ASTa
Waziri John Kerry na mwenzake wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Saud Al-Faisal bin Abdulaziz al-Saud.
Waziri John Kerry na mwenzake wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Saud Al-Faisal bin Abdulaziz al-Saud.Picha: Jacquelin Martin/AFP/Getty Images

Saudi Arabia imekasirishwa na sasa imedeokeza kuwa itajaribu kujenga mahusiano na nchi nyingine mbali ya zile za magharibi. Na iwapo itajaribu kuingia katika harakati za kuunda silaha za nyuklia nchi hiyo itakuwa katika hatari ya kutengwa. Marekani ndiyo mshirika wa pekee anaeweza kuvilinda visima vya mafuta vya Saudi Arabia. Kwa hiyo nchi hiyo haina mawezekano makubwa katika kuchagua kutekeleza siasa ya mambo ya nje.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akihutubia mkutano wa waandishi na mwenzake wa Saudia, mwanamfalme Saud Al-Faisal bin Abdulaziz al-Saud mjini Riadhi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akihutubia mkutano wa waandishi na mwenzake wa Saudia, mwanamfalme Saud Al-Faisal bin Abdulaziz al-Saud mjini Riadhi.Picha: Reuters

Mahusiano ya kijeshi na mataifa mengine
Kutokana na kukasirishwa na Marekani maafisa waandamizi wa Saudi Arabia wamedokezea juu ya mawezekano ya kujenga mahusiano ya kijeshi na mataifa mengine duniani licha ya nchi za magharibi, kwa lengo la kudumisha msimamo mkali dhidi ya washirika wa Iran katika eneo la arabuni na linalopakana nalo, ikiwa mataifa ya dunia yatashindwa kuizuia mipango ya nyukilia ya Iran. Maafisa hao pia wamezungumzia juu ya uwezekano wa Saudi Arabia kuwa na silaha za nyuklia.

Lakini washirika wengine kama Marekani ni vigumu kwa Saudi Arabia kuwapata hasa kutokana na kutambua kwamba Saudi Arabia ni mshirika mkubwa wa Marekani wa tokea miaka mingi sana. Kwa sasa Urusi imesimama na Rais Bashar al -Assad katika vita vya nchini Syria wakati Saudi Arabia inawaunga mkono waasi. Na uwezo wa kijeshi wa China ni mdogo kulinganisha na ule wa Marekani.

Ni vigumu kujitoa kwa Marekani
Bwana Robert Jordan aliekuwa balozi wa Marekani nchini Suadi Arabia kuanzia mwaka wa 2001 hadi 2003 amesema, kuwa patakuwapo na mipaka katika ushirika wowote ambao Saudi Arabia itajaribu kuujenga na nchi nyingine. Balozi huyo amesema hakuna nchi nyingine yoyote duniani yenye uwezo wa kuyalinda mafuta ya Saudi Arabia na uchumi wa nchi hiyo kuliko Marekani na Saudi Arabia inayatambua hayo.

Wakati bwana Robert Jordan alikuwa ni mwanadiplomasia wakati wa utawala wa Rais George W. Bush wachambuzi wa masuala ya Saudi Arabia pia wamesema kwamba nchi hiyo ya kifalme inatambua vizuri athari zinazoweza kutokea kwake ikiwa itaibadilisha sera yake ya mambo ya nje na hasa ikiwa itajaribu kuundaa silahaa za nyuklia.

Uhusiano wa kihistoria. Rais wa zamani wa Marekani D. Roosevelt alipokutana na Mfalme Saud wa Saudia Arabia mwaka 1945.
Uhusiano wa kihistoria. Rais wa zamani wa Marekani D. Roosevelt alipokutana na Mfalme Saud wa Saudia Arabia mwaka 1945.Picha: picture alliance/akg-images

Haitaki kuwa Iran nyingine
Ikiwa itafanya hivyo nchi hiyo itaonekana kuwa jahili wa kimataifa badala ya kuonekana kuwa adui mkubwa wa Iran. Ni wazi kwamba Saudi Arabia haitaki kujiingizaa katika hali kama hiyo iliyoilazimisha Iran kwenda kwenye mazungumzo.

Mchambuzi mmoja kutoka Saudi Arabia amesema nchi hiyo asilani haihitaji kuwa Iran nyingine. Amesema kufanya hivyo kutakuwa kinyume kabisa na maadili ya Saudi Arabia, kwa kutambu kwamba nchi hiyo mshirika mwaminifu katika jumuiya ya kimataifa, na pia ni nchi inayotoa mchango mkubwa katika kuimarisha utulivu na kuyaimarisha masoko ya mafuta. Duru za kidiplomasia na wachambuzi kutoka nchi za ghuba wanasema Saudi Arabia haitadiriki kuvunja uhusiano wake na Marekani.

Mwandishi: Mtullya abdu/rtre
Mhariri:Saum Yusuf