1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SERBIA KOSOVO.Serbia yapinga mpango wa umoja wa mataifa

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCS4

Bunge la Serbia limepinga mpango wa umoja wa mataifa uliokuwa unapendekeza kutolewa uhuru wa kadiri kwa jimbo lililojitenga la Kosovo.

Mswaada huo wa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Marti Ahtisaari ulipigiwa kura bungeni na kukataliwa kwa kura 225 dhidi ya kura 15.

Wabunge wa Serbia pia wamepitisha azimio na kusema kwamba mpango huo unakiuka sheria za kimataifa.

Hata hivyo pendekezo hilo la umoja wa mataifa limeungwa mkono na viongozi wa Kosovo wenye asili ya Kialbania.

Kosovo imekuwa chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa tangu kampeni ya mabomu ya NATO ya mwaka 1999 kumaliza mapigano kati ya serikali ya Yugoslav na wanajeshi wenye asili ya Kialbania.