1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serbia yainyamazisha Ujerumani

Aboubakary Jumaa Liongo18 Juni 2010

Safari ya Ujerumani katika fainali za kombe la dunia imeingia ugumu hii leo baada ya kufungwa na Serbia

https://p.dw.com/p/NwpY
Golikipa wa Serbia Vladimir Stojkovic akiokoa mkwaju wa penalti uliyopigwa na Lukas Podolski, kuliaPicha: AP

Ujerumani ambayo ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kutwaa kombe la dunia, leo imefungwa bao 1-0 na Serbia katika mechi ambayo ilishuhudia Ujerumani ikicheza na wachezaji kumi kwa muda mrefu wa mchezo.

Ujerumani ambayo katika mechi ya kwanza iliifunga Australia mabao 4-0, ilishuhudia mchambuliajai wake Miroslva Klose akipewa kadi nyekundu, na pia Lukas Podoski akikosa penalti.

Mechi nyingine hii leo ni kati Marekani na Slovenia kabla ya Uingereza kucheza na Algeria.

Mwandishi:Aboubakary Liongo