1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serbia yakanusha madai ya kuigawanya Kosovo

21 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DSRO

BELGRADE

Rais wa Serbia,Boris Tadic, amekanusha madai kuwa utawala wa Belgarde unataka kuigawanya Kosovo,ambayo ilijitangazia uhuru wake kutoka Serbia mwzi uliopita.

WaSerb wa Kosovo walipambana na vikosi vya NATO pamoja na vya Umoja wa Matiafa katika mji ambao umegawanyika kikabila wa Mitrovica.Ghasia zilitokea wiki iliopita,kuleta wasiwasi kuwa huenda Belgrade inapanga kupanua utawala wake hadi kaskazini mwa Kosovo.

Kwa mda huohuo Urusi imeikosoa Marekani kwa mipango yake ya kuipa silaha Kosovo.Waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa mipango ya serikali ya Marekani inakiuka azimio la Umoja wa Mataifa ambalo linaruhusu tu silaha kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa ya Kosovo.Vyombo vya habari vya Urusi vinasema kuwa serikali ya Moscow inapanga kuchukua suala hilo katika kikao maalum na NATO.Washington imepinga wasiwasi uliopo kuwa msaada wa kijeshi kwa taifa changa la Kosovo kutahatarisha usalama wa eneo hilo.Ikulu ya White House ,kupitia taarifa ,imesema kuwa Kosovo ina haki ya kuwa na jeshi japo dogo chini ya mpango wa kujitegemea ulioratibiwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa,Martii Ahtisaari.