1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serbia yaupa masharti umoja wa Ulaya.

4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CkEH

Belgrade. Waziri mkuu wa Serbia Vojislav Kostunica amesema kuwa umoja wa Ulaya unapaswa kuchagua baina ya kutia saini mkataba na Serbia ama kuweka ujumbe wake katika jimbo la Kosovo. Amesisitiza kuwa kutuma ujumbe wa umoja wa Ulaya katika jimbo la Kosovo bila ya maridhiano na Serbia kutaathiri mahusiano ya umoja huo na taifa hilo la Balkan. Umoja wa Ulaya , ukiungwa mkono na Marekani, unapanga kutuma ujumbe wa polisi 1,800, maafisa wa forodha na mahakama kusaidia hatua za kwanza za Kosovo kama taifa huru. Kosovo inatarajiwa kutangaza uhuru muda mfupi baada ya uchaguzi wa duru ya pili wa rais nchini Serbia hapo February 3. Serbia inasisitiza kuwa Kosovo itabaki kuwa sehemu ya ardhi yake.