1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali mpya Ugiriki

9 Novemba 2011

Mazungumzo ya kuunda serikali mpya ya mpito nchini Ugiriki yanatarajiwa kuendelea hii leo huku kukisubiriwa kutangazwa waziri mkuu mpya

https://p.dw.com/p/1378h
Waziri mkuu George Papandreou kulia, akiwasili kwenye mazungumzo ya kuunda serikaliPicha: dapd

Serikali mpya ya mpito Ugiriki itatangazwa hii leo.Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo.

Einigung über Bildung einer Übergangsregierung in Griechenland
Waziri mkuu wa Ugiriki George PapandreouPicha: dapd

Mazungumzo yalioingia siku ya tatu ya kuunda serikali hiyo mpya yalisita hapo jana jioni, pasi kutajwa waziri mkuu mpya atakaye mrithi yule anayeondoka, Gerge Papandreou. Papandreou na kiongozi wa upinzani Antonis Samaras, walifanya mazungumzo siku nzima ya Jumatatu.

Loukas Papademos
Loukas PapademosPicha: picture-alliance/dpa

Aliyekuwa makamu wa rais wa benki kuu ya Ulaya, Lucas Papademos, huenda ndiye atakayekuwa waziri mkuu mpya. Papandreou amekubali kujiuzulu punde tu makubaliano yatakapofikiwa.

Serikali ya mpito itakuwa na jukumu la kutekeleza mageuzi yalioitishwa na Umoja wa Ulaya na shirika la kimataifa la fedha, IMF, ili nchi hiyo inayokumbwa na madeni iweze kupokea mkopo.

Mwandishi Maryam Abdalla/all