1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali mpya ya Tunisia yakutana

Kabogo Grace Patricia21 Januari 2011

Serikali mpya ya mpito nchini Tunisia jana imefanya mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri.

https://p.dw.com/p/100J5
Rais wa mpito wa Tunisia, Fouad MebazaaPicha: AP

Mkutano huo umefanyika huku maandamano mapya ya kutaka kuondolewa viongozi wa serikali iliyopita ya rais aliyeondolewa madarakani, Zine El Abidine Ben Ali, yakiendelea.

Kabinettssitzung Interimsregierung Tunesien
Rais wa Tunisia, Fouad Mebazaa, wa pili kulia akiongoza kikao cha kwanza cha mawaziriPicha: AP

Mawaziri hao wamekubaliana kutoa msamaha kwa wafungwa wote wa kisiasa na kuvihalalisha vyama vya siasa na makundi yaliyokuwa yamepigwa marufuku.

Wakati huo huo, polisi katika mji mkuu wa Tunis, wamefyatua risasi za onyo kuwatawanya mamia ya waandamanaji karibu na makao makuu ya kilichokuwa chama tawala.

Mmoja kati ya wapinzani wakuu wanaoongoza nchini humo, Taoufik Ben Brik, ametangaza kugombea katika uchaguzi wa rais ambao serikali ya mpito imesema utakuwa huru na wa haki.