1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya chama cha Kiisilamu Tunisia kujiuzulu

29 Septemba 2013

Chama kikuu cha wafanyakazi nchini Tunisia UGTT kimekuwa mpatanishi katika mazungumzo ya mzozo nchini humo jana (27.09.2013) ambapo chama tawala cha Ennahda kimekubali mpango wa mazungumzo ya kuunda serikali mpya.

https://p.dw.com/p/19q53
Members of constituent assembly listen to Tunisian Prime Minister Hamadi Jebali, standing at right, as he presents his government in Tunis, Thursday, Dec. 22, 2011, while Assembly President, Mustapha Ben Jaafar, 2nd right, looks on in Tunis, Thursday, Dec. 22, 2011. Jebali presented his coalition government, giving some key ministries to a moderate Islamist party, which dominated the country's first post-uprising elections. The new coalition Cabinet presented Thursday, is the first since the country's first post-uprising elections. (Foto:Hassene Dridi/AP/dapd)
Baraza la kutunga sheria la TunisiaPicha: AP

Chama hicho kikuu cha wafanyakazi nchini humo kiliitisha mkutano kati ya chama hicho kinachofuata nadharia za dini ya Kiislamu pamoja na upinzani usiopendelea dini kuwa msingi wa maadili ya jamii ili kukubaliana juu ya tarehe wiki ijayo ambapo kutafanyika mjadala wa kitaifa, wenye lengo la kumaliza mzozo uliozushwa na mauaji ya mbunge maarufu wa upande wa upinzani Julai mwaka huu.

The leader and founder of the moderate Islamic party Ennahda, Rached Ghannouchi, adresses the media during a press conference held in Tunis, Thursday, Oct. 28, 2011. Tunisia's moderate Islamist party Ennahda, banned for decades, emerged the official victor in the nation's first free elections, taking 41.47 percent of the vote and 90 of 217 seats in an assembly that will write a new constitution, the electoral commission announced. (Foto:Hassene Dridi/AP/dapd)
Muasisi na kiongozi wa chama cha Ennahda Rached GhannouchiPicha: dapd

Vuguvugu la mapinduzi ya umma

Nchi hiyo ambayo ni chanzo cha vuguvugu la mapinduzi katika mataifa ya Kiarabu mwaka 2011 imetumbukia katika mzozo wa kisiasa , wakati upande wa upinzani usiopendelea dini kuwa msingi wa maadili ya umma ukikishutumu chama cha msimamo wa wastani cha Ennahda kwa kushindwa kuwadhibiti watu wenye itikadi kali ya dini ya Kiislamu.

Katika taarifa iliyochapishwa katika tovuti yake chama hicho cha wafanyakazi cha UGTT, ambacho kimekuwa na uhusiano usiokuwa mzuri na chama cha Ennahda na hapo kabla kukishutumu chama hicho kwa kuburuza miguu katika hatua za mageuzi nchini humo, kimesema kuwa chama hicho tawala kimekubali mpango wake wa mpito.

epa02977467 Tunisians wait in a line on 23 October 2011 to cast their votes. Tunisians go to the polls Sunday in the country's first ever free elections, nine months after a revolution that forced out the country_s dictator, setting an example for the entire Arab world. Around 11,000 candidates are competing in the election of a 217-member constituent assembly, which will draw up a new constitution, under which presidential and parliamentary elections will be held. EPA/STRINGER
Wapiga kura nchini TunisiaPicha: picture-alliance/dpa

"Taasisi hiyo inayodhamini mpango huo inakaribisha matokeo hayo na inatoa wito kwa vyama vyote kujiunga na majadiliano ili kuteua tarehe kwa ajili ya mjadala wa kitaifa," kimesema chama hicho, na kuongeza kuwa kinamatumaini ya kuitisha mkutano huo baadaye wiki ijayo. Chama cha wafanyakazi cha UGTT hapo kabla kimetoa wito wa kufanya kampeni ya upinzani kuhakikisha kuwa chama cha Ennahda kinakubaliana kikamilifu na mpango wake huo wa mpito.

Shutuma

Chama hicho kimekishutumu chama cha Ennahda kwa kufanya kila kiwezacho kuhakikisha kushindwa kwa mpango huo, ambao kimeutayarisha pamoja na chama cha waajiri Utica, shirika lisilokuwa la kiserikali la kutetea haki za binadamu nchini humo la Tunisia League for Human Rights , pamoja na chama cha wanasheria.

Ennahda imekataa mabadiliko, na inaushutumu upinzani ambao kwa kiasi kikubwa unapinga dini kuwa msingi wa maadili, kwa kuvuruga mapendekezo ya wapatanishi kwa kudai serikali ijiuzulu mara moja. Mpango huo umeweka muda wa wiki tatu kwa kuundwa baraza la mawaziri litakalokuwa na wajumbe ambao si wanasiasa litakalochukua nafasi ya serikali ya sasa, baada ya kuanzishwa kwa majadiliano na vyama vya upinzani.

epa02979458 Supporters of Islamist Ennahda party attend a announcement by members of their party to media at the party's headquarters in Tunis, Tunisia, on 24 October 2011. Tunisia's moderate Islamist party Ennahda claimed victory in the country's historic first free elections, saying that unofficial results gave it the lion_s share of the vote. 'The first confirmed results show that Ennahda has obtained first place nationally and in most districts,' the party's campaign manager, Abelhamid Jelassi, told a press conference a day after the first democratic elections in the birthplace of the Arab Spring. EPA/STR +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wafuasi wa chama cha Ennahda-nchini TunisiaPicha: picture-alliance/dpa

Pia limeweka muda wa wiki nne wa kuidhinishwa kwa sheria mpya za uchaguzi, na kuweza muda maalum wa uchaguzi mpya na kukamilisha mswada wa katiba mpya ambao umecheleweshwa kwa muda mrefu. Msemaji wa chama cha Ennahda Lajmi Lourimi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa chama chake "kiko tayari kuingia katika majadiliano na vyama vyote ambavyo vitapenda". "Mjadala wa kitaifa unaweza kuanza wiki ijayo, lakini hakuna tarehe iliyokwisha pangwa."

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Bruce Amani