1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya China yakiri polisi walifyatua risasi dhidi ya watibet

21 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DS9D

BEIJING

Kwa mara ya kwanza serikali ya China imekiri kwamba jeshi lake la polisi liliwafyatulia risasi na kuwajeruhi waandamanaji wanne jumapili iliyopita wakati wa maandamano ya watibet dhidi ya serikali hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la China Xinua.

Viongozi wa Tibet walioko uhamishoni wamesema kwamba kiasi cha watu 100 inaaminika waliuwawa kwenye harakati za polisi wa China za kuyazima maandamano.Wakati huohuo kuna ripoti zinazosema kwamba China imepeleka maelfu ya wanajeshi wake katika jimbo la Tibet na majimbo mengine ya karibu katika juhudi za kukomesha ghasia zinazoendelea.Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa China Yang Jiechi ambapo ameitolea mwito serikali ya China kujizuia kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji na kuanza mazungumzo na kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama anaishi uhamishoni.Dalai Lama amewataka watibet kumaliza ghasia na amesema yuko tayari kukaa chini kwa mazungumzo na serikali ya China.