1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imepinga vikali matamshi ya Balozi wa Ujerumani mjini Kinshasa

29 Machi 2007

Walinzi wa kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean Pierre Bemba katika jimbo la Equater(Ikwater) wamesalimisha silaha zao na kujiunga na jeshi la taifa.

https://p.dw.com/p/CHHC
Mji wa Kinshasa,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Mji wa Kinshasa,Jamhuri ya Kidemokrasi ya KongoPicha: Alexander Göbel

Hatua hiyo inafuatia mapigano ya wiki iliopita kati ya walinzi wa Bemba mjini Kinshasa na majeshi ya serikali, mapigano yaliosababisha vifo vya zaidi ya watu 150. Wakati huo huo serikali ya nchi hiyo imeyapinga vikali matamshi ya balozi wa Ujeruamni mjini Kinshasa kwamba ilitumia nguvu pasipohitajika.

Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo kutoka Kinshasa ametuletea ripoti kamili.