1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Kenya kudhibiti mfumuko wa bei

11 Mei 2017

Wabunge kwa wingi wameunga mkono mswaada wa fedha ambao ukipitishwa utawezesha kushusha gharama ya juu ya maisha inayoshuhudiwa wakati huu. Bei za vyakula zimepanda kwa kasi katika siku zilizopita.

https://p.dw.com/p/2cml6
Soko
Picha: picture-alliance/dpa/G. Esiri

Gharama ya Maisha Kenya - MP3-Stereo

Wakati huo huo wafanyibiashara walaghai wamelaumiwa kwa kuficha bidhaa muhimu na kusababisha uhaba mkubwa wa bidhaa hizo katika masoko na maduka. Wananchi wa tabaka la chini wanalalamika juu ya ongezeko la bei za bidhaa kama unga, sukari na maziwa.

Wakenya wanaoathirika na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu huenda wakapata afueni baada ya Bunge kuunga mkono mswaada wa fedha uliowasilisha kwa mara ya pili bungeni. Wakenya wengi wanalalamika juu ya kupanda kusiko kwa kawaida kwa ghama za maisha.

Utakapopitishwa m swaada huo utaiwezesha serikali kuagiza bidhaa za vyakula kwa bei nafuu kutoka nchi za nje na vilevile kudhibiti bei za bidhaa muhimu kama mahindi sukari na vyakula vingine na hivyo kupunguza gharama za maisha ambazo zimepanda kwa kiwango cha juu katika muda wa miezi miwili iliyopita. Uhaba wa mahindi nchini Kenya umesababisha kupanda kwa bei ya unga kwa zaidi ya asilimia 100.