1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Kenya kupinga uamuzi wa mahakama kuhusu Haiti

Tatu Karema
27 Januari 2024

Serikali ya Kenya imeapa kupinga uamuzi wa mahakama dhidi ya hatua yake ya kutaka kutuma kikosi cha polisi nchini Haiti kuongoza ujumbe wa kudumisha sheria na utaratibu unaoungwa mkono na UN

https://p.dw.com/p/4bjmJ
Mahakama ya juu nchini Kenya
Mahakama ya juu nchini KenyaPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Jaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya Enock Chacha Mwita, ameamua kwamba "uamuzi wowote wa chombo chochote cha serikali ama afisa wa serikali wa kupeleka kikosi cha polisi nchini Haiti unakiuka katiba na sheria hivyo basi ni kinyume cha sheria.''

Soma pia:Mahakama Kenya yaizuwia serikali kupeleka askari Haiti

Saa chache baadaye, msemaji wa serikali Isaac Mwaura alijibu kwa kusema kuwa wakati serikali inaheshimu utawala wa sheria, imefanya uamuzi wa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo mara moja.

Soma pia:Bunge la Kenya yaidhinisha polisi kutumwa nchini Haiti

Mwaura ameongeza kuwa serikali inasisitiza kujitolea kwake katika kuheshimu majukumu yake ya kimataifa.

Huku hayo yakijiri, Ekuru Aukot, mwanasiasa wa upinzani aliyepinga hatua ya kupelekwa kwa kikosi hicho cha polisi nchini Haiti, amesema yuko tayari kwa mapambano ya muda mrefu.