1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Kenya yaimarisha ulinzi

30 Januari 2013

Wakati Kenya ikijiandaa kuingia katika uchaguzi mkuu, suala la usalama limekuwa ni agenda muhimu nchini humo kufuatia matukio mbali mbali ya ghasia yaliyojitokeza wiki za hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/17Twl
Msemaji wa serikali ya Kenya, Muthui Kariuki.
Msemaji wa serikali ya Kenya, Muthui Kariuki.Picha: DW/R. Kyama

Ni kutoka na hilo msemaji wa Serikali ya nchi hiyo Muthui Kariuki amekuwa na mkutano na waandishi habari leo na kusema kwamba serikali ya nchi hiyo imejiandaa vilivyo kwa uchaguzi wa tarehe 4 Machi, hususan kuhusu suala hilo la usalama. Mwandishi wetu Reuben Kyama ametuma taarifa ifuatayo na ili uweze kusikiliza bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.


Mwandishi: Reuben Kyama
Mhariri: Saumu Yusuf
 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi