1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Kenya yawataka madaktari kusitisha mgomo wao

Tatu Karema
3 Aprili 2024

Serikali ya Kenya imetoa wito kwa madaktari nchini humo kusitisha mgomo wao wa kitaifa ambao sasa umeingia wiki ya tatu na kulemaza huduma za afya katika baadhi ya hospitali za umma

https://p.dw.com/p/4eMrd
Mgomo wa madaktari uliofanyika nchini Angola mnamo Desemba 6, 2021
Mgomo wa madaktari nchini AngolaPicha: Ndomba, Borralho/DW

Katika taarifa iliyotolewa jana na kutiwa saini na mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, serikali ya kenya imesema kuwa itatimiza baadhi ya matakwa ya madaktari hao.

Matakwa ya madaktari yatakayotekelezwa 

Matakwa hayo ni pamoja na malipo ya malimbikizi chini ya makubaliano ya pamoja ya mwaka 2017, na kuwekwa kwa bajeti ya kuajiri madaktari wakufunzi miongoni mwa masuala mengine.

Soma pia:Mgomo wa madaktari waathiri hospitali za umma Kenya

Serikali hiyo imesema kuwa inataka kutatua mzozo wa sasa na kumaliza kabisa migomo katika sekta ya afya.

Taarifa hiyo, imeutaka uongozi wa chama cha madakatri nchini humo KMPDU kuzingatia majukumu yake chini ya agizo la mahakama la mwezi uliopita la kusitisha mgomo huo.

KMPDU imeapa kuendeleza mgomo

Viongozi wa chama hicho wameapa kuendelea na mgomo huo licha ya agizo hilo la mahakama.