1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Uganda na kundi la LRA wakubaliana kurejea katika meza ya mazungumzo

17 Aprili 2007

Serikali ya Uganda na kundi la waasi la Lords Resistance Army LRA wametia saini makubaliano mapya ya amani mwishoni mwa juma na kukubali kurejea katika meza ya mazungumzo baadaye mwezi huu.

https://p.dw.com/p/CHGA
Kiongozi wa LRA Joseph Kony
Kiongozi wa LRA Joseph KonyPicha: AP

Kwa mujibu wa msemaji wa kundi hilo kiongozi wa LRA Joseph Kony alishuhudia kutiwa saini makubaliano hayo katika eneo la Ri-Kwangba nchini Sudan. Joseph Kony anachelea kuonekana kwa kuhofia kukamatwa na kupelekwa The Hague Uholanzi ili kujibu mashtaka ya kuhusika na uhalifu wa kivita. Pande zote mbili zilitia makubaliano ya amani mwezi Agosti na mazungumzo kukwamishwa na vitendo vya uhasama.

Mwandishi wetu Omar Mutasa anaarifu zaidi kutoka Kampala.