1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali yavunjwa Côte d'Ivoire

Oumilkheir Hamidou
19 Julai 2017

Rais Alassane Outtara wa Côte d'Ivoire amewabadilisha mawaziri wake wa ulinzi, bajeti na mambo ya ndani alipolivunja baraza lake la mawaziri.

https://p.dw.com/p/2gokX
Elfenbeinküste Meuternde Soldaten an einem Checkpoint
Picha: Reuters/L. Gnago

Nchi hiyo inayozalisha kakao kwa wingi zaidi ulimwenguni imejikuta mwaka huu ikisumbuliwa na uasi wa mara kwa mara wa wanajeshi, matukio yaliyogharimu mamia kwa mamilioni ya fedha walizobidi kulipwa wanajeshi hao na kwa namna hiyo kuchafua sifa ya Côte d'Ivoire ya baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hamed Bakayoko, mtu wa karibu sana na rais Ouattara, aliyekuwa hapo awali waziri wa mambo ya ndani amekabidhiwa wizara ya ulinzi, kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na katibu mkuu wa ofisi ya rais Patrick Achi mbele ya maripota, kabla ya mkutano wa baraza la mawaziri.

Wakati huo huo Sidiki Diakite aliyekuwa hadi sasa meya wa jiji la Abidjan ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Waziri mkuu Amadou Gon Goulibaly atakabidhiwa wizara ya bajeti akisaidiwa na Moussa Sanoogo kama katibu wa dola. Waziri wa zamani wa bajeti Abdourahmane Cisse ameteuliwa kuwa mshauri maalumu wa rais Ouattara.

Rais Alassane Ouattara wa Côte d'Ivoire
Rais Alassane Ouattara wa Côte d'IvoirePicha: REUTERS/T. Gouegnon

Mapigano ya mwishoni mwa wiki ndio chanzo cha kuvunjwa baraza la mawaziri

Waziri wa zamani wa ulinzi Alain-Richard Donwahi amekabidhiwa hivi sasa wizara ya maji na misitu.

Itafaa kusema kwamba wanajeshi watatu waliuliwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi iliyopita risasi zilipofyetuliwa katika kambi ya kijeshi ya Korhogo, kaskazini mwa Côte d'Ivoire. Duru za karibu na jeshi zinasema tukio hilo lilikuwa jibu kwa uasi wa kijeshi ulioigubika nchi hiyo miezi ya January na Mei mwaka huu."Maluteni wa kijeshi ndio waliokuwa chanzo cha kisa hicho lakini hadi wakati huu sababu haijulikani" duru hizo za kijeshi zimeeleza.

Mwezi january na mai mwaka huu waasi wa zamani waliojumuishwa jeshini walifanya uasi, lakini walisitisha uasi wao walipolipwa kila mmoja Euro 18.000. Kwa jumla walikuwa wanajeshi 8400. Mzozo huo uliidhofisha mno serikali ya Côte d'Ioire na hasa rais wake Alassane Ouattara ambae sifa zake zimeanza kuingia dowa.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/Reuters

Mhariri:Josephat Charo