1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEVELLE.Urusi yapinga hatua ya kuipa uhuru Kosovo

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTh

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Ivanov ameonya juu ya hatua ya kupewa uhuru jimbo la Kosovo kuwa ni sawa na kuanzisha harakati za kudai uhuru kwa majimbo mengine yaliyokuwa chini ya utawala wa ki-Sovieti.

Maoni ya waziri Ivanov yanakwenda kinyume na tamko la mawaziri wenzake wa nchi wanachama wa shirika la kujihami la NATO katika mkutano wao unaofanyika mjini Seville, Uhispania ambalo linaunga mkono mpango wa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Marti Ahtisaari unaopendekeza Kosovo iandaliwe kupata uhuru kutoka kwa Serbia chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa.

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Ivanov alisema.

O ton……Ikiwa tunafikiria hali ambapo eneo la Kosovo litapewa uhuru basi majimbo mengine pia yatataka yapewe uhuru wao.

Na hayo sio tu kwa yale majimbo yaliyokuwa chini ya utawala wa ki- Sovieti bali ni katika ulaya nzima, kwa hivyo lazima tuwe waangalifu.

Mjumbe maalum Marti Ahtisaari anatarajiwa kuwasilisha mapendekezo yake mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa wiki ijayo.