1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEVILLE : NATO yaitathmini Afghanistan

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTp
Heidermarie Wieczoreck-Zeul (kushoto) na Robert Zoellick
Heidermarie Wieczoreck-Zeul (kushoto) na Robert ZoellickPicha: AP

Katika mazungumzo ya mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO yanayofanyika mjini Seville nchini Uhispania Marekani inawashinikiza washirika wenzake wa Ulaya kupeleka wanajeshi zaidi nchini Afghanistan kuzima shambulio la Taliban linalotegemewa wakati wa majira ya chipukizi.

Marekani na Uingereza zimeahidi kutowa wanajeshi wa ziada 3,000 kwa kikosi cha wanajeshi 35,000 wa NATO lakini mataifa mengine yakiwemo Uholanzi,Ufaransa na Uturuki yamekataa kutuma wanajeshi zaidi.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Yung amesema badala ya kutumwa kwa wanajeshi zaidi ni muhimu kuimarisha usalama na juhudi za kuijenga upya nchi hiyo.

Ujerumani ina wanajeshi 2,300 katika shughuli zisizo za mapigano ambapo zaidi wanashughulikia kazi za kuijenga upya nchi hiyo kaskazini mwa Afghanistan lakini wiki hii imethibitisha kutuma ndege sita za upelelezi kupiga doria eneo tete la kusini mwa Afghanistan ambapo wiki iliopita wanamgambo waliuvamia mji wa Musa Qala.

Mawaziri hao wanaokutana Seville pia watajadili shughuli nyengine kuu ya NATO huko Kosovo.