1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shabaha za mradi wa Millennium kwa Tanzania

24 Aprili 2007

Mradi wa Millennium kwa nchi kama Tanaznia haufahamiki na wananchi wake wengi kuwa ni kuwakomboa wao kutoka umasikini.

https://p.dw.com/p/CHFY

Wakati mradi wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya millennium ni fikra njema , ajenda iliojificha nyuma ya mradi huo ya nchi za magharibi, inafanya kuwa taabu kwa nchi za kiafrika kama Tanzania kufikia shabaha zake.

Huu ni Uchambuzi wa Rashid Mkwinda,mchezaji wa kuigiza:

Mkwinda ni mmoja kati ya watu walioulizwa maoni yao na shirika la habari la IPS katika mitaa ya Dar-es-salaam kuhusu mradi huo wa maendeleo wa millennium.Kwa jicho lake, uwezo wan chi za kusini mwa Afrika kufikia shabaha za iliennium unahusiana na sera za dola kuu kwa nchi changa zinazoinukia.

Mkwinda anajiuliza iwapo mradi wa millennium sio sawa na miradi mingine ya kimataifa ambayo yanalenga kutumia nguvu zao kuzidhibiti nchi masikini na kunyonya raslimali ya nchi za kiafrika.

Mkwinda asema na ninamnukulu,

“Ni dhahiri kwamba Marekani na marafiki zake inataka kunyonya raslimali zetu kwavile bado hatuna sauti sawa na wao katika kutekeleza miradi hiyo ya millennium.”

Akaongeza kwa kuuliza iwapo miradi hii ya millennium, haifanyi kazi kama ile ya kikoloni yenye shabaha ya kuwawekea viongozi wa nchi za kiafrika kanuni na masharti mapya.

Kwani, anadai, UM unatum,iwa na mataifa makuu machache kutekeleza masilahi yao ya pamoja-asema Mkwinda.

Mbali na Mkwinda ,sehemu kubwa ya watu walioulizwa maoni yao mitaani hawajui mengi kuhusu shabaha 8 za mradi huo wa millennium ambazo zinanzia kupunguza umasikini kwa nusu hadi ifikapo 2015 hadi kuondosha ukosefu wa usawa ulimwenguni.

Mchuuzi wa bidhaa barabarani John Kasmuni, anakanusha kuwa watanzania hawafuatili kipitacho ulimwenguni,lakini anaungama wengi wao hawajui mengi kuhusu shabaha halisi za mradi wa Millennium.ALISEMA NA NINAMNUKULU,

“SIJAJUA KABISA KWAMBA MRADI HUO UMETUHUSI SISI MASIKINI”.

Ukitupa barabara juu ya miradi ya shabaha za Millennium yathibitisha kwamba Tanzania itakumbana kweli na shida kutimiza shabaha hizo.Shabaha ya 6 nayo ni kuzuwia kutapakaa kwa maradhi ya ukimwi na malaria uko mbali sana kuweza kufikiwa na Tanzania.

Kwani, kwa muujibu wa tarakimu za 2006 za wizara ya afya ,kiasi cha watanzania laki moja hufariki kila mwaka kutokana na maradhi ya malaria.Kiasi cha 70% ya wale wanaofariki, ni watoto wadogo chini ya umri wa miaka 5.

Athari zake kiuchumi ni kuwa 40% ya fedha za umma katika matumizi ya afya zinalenga kupiga vita malaria wakati 50% za wagonjwa wanaopokewa hospitalini waugua malaria.

Kuna watanzania wanaona shabaha za mradi wa Millennium zaweza kufikiwa.Mmoja wao ni Nazareth Neto.Anafurahia hatua iliopiga serikali ya Tanzania katika ujenzi wa mashule kwani, hii itaongeza idadi ya wanafunzi.Serikali, anasema, imeanzisha pia elimu bure ya shule za msingi.

Na tarakimu zaonesha watoto walioandikisha mashuleni kwa mwaka wa darasa la kwanza ilisalia vile vile baina ya 1995 na 1999.Lakin, ilionegezeka kati ya 2001 na 2004.

Serikali pia imefanya mradi wa kujenga shule zaidi za sekondari ili kukabili upungufu wa shule za aina hiyo.

Hatahivyo, serikali ya Tanzania, haikutenda ya kutosha kunyanyua hali za kimaisha za walimu,amesema Ellen Binagi,mratibu wa mipango ya elimu katika shirika la misaada la Oxfam.Matokeo yake , walimu zaidi yamkini wakaacha kazi ya uwalimu na kusaka kazi nyengine wakipata upenu mdogo tu kufanya hivyo.