1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la guruneti Rwanda

Josephat Nyiro Charo12 Agosti 2010

Watu saba wamejeruhiwa

https://p.dw.com/p/Oj3N
Jiji la KigaliPicha: Ch.Kaess

Shambulio la guruneti limeutikisa mji mkuu wa Rwanda, Kigali jana , na kuwajeruhi kiasi watu saba wakati rais Paul Kagame akitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambao umekosolewa sana kwa kukosa upinzani wa kweli.

Msemaji wa polisi kepteni Eric Kayiranga ameliambia shirika la habari la AFP kuwa guruneti lilitupwa karibu na kituo kikuu cha mabasi mjini Kigali, saa chache baada ya rais Kagame kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatatu kwa ushindi wa kishindo kufuatia kampeni iliyofanyika huku wapinzani wakikamatwa pamoja na mauaji.

Watu kiasi saba wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watoto, na watuhumiwa watatu wamekamatwa. Mwandishi habari kutoka Marekani Steve Terril , ambaye alikuwa katika eneo hilo wakati guruneti hilo lilipolipuka , amesema kuwa ameona kiasi watu 20 ambao wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mwanamke ambaye amepoteza jicho.