1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la bomu Lebanon limeua watu wanne

26 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cxvd

BEIRUT: Nchini Lebanon,si chini ya watu 4 wameuawa mjini Beirut katika mripuko mkubwa wa bomu lililotegwa ndani ya gari.Miongoni mwa wale waliouawa ni Wisam Eid aliekuwa afisa katika idara ya upelelezi na kujulikana kama mshirika wa Saad al-Hariri anaeongoza serikali ya ushirikiano inayoipinga Syria.Eid alihusika na uchunguzi unaoongozwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Rafik al-Hariri aliekuwa waziri mkuu wa Lebanon na baba wa Saad al-Hariri.

Lebanon inajikuta bila ya rais tangu muhula wa Emile Lahoud anaeelemea upande wa Syria,kumalizika miezi miwili iliyopita.Saad al-Hariri anailaumu serikali ya Damascus kuwa inachochea mgogoro unaohusika na uteuzi wa rais.