1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la kigaidi laua wanajeshi 29 Niger

Sudi Mnette
4 Oktoba 2023

Utawala wa kijeshi nchini Niger umesema wanajeshi wake 29 wameuwawa kwa shambulizi la magaidi karibu na mpaka wa taifa hilo na Mali.

https://p.dw.com/p/4X5Ac
Nigeria | Explosion illegale Ölraffinerie
Picha: AP Photo/picture alliance

Waziri wa Ulinzi wa Niger, Luteni Jenerali Salifou Mody, amesema zaidi ya wapiganai 100 wanaotumia mabomu ya kuundwa nyumbani, wamekuwa wakiwalenga walinzi wa usalama wa taifa hilo ambao wapo katika ulinzi wa mpakani.

Hili ni shambulio la pili lenye kuwalenga wanajeshi wa Niger kwa juma hili pekee.

Hata hivyo Mody alionesha hali kudhibitiwa na nyenzo zao za vita kuteketezwa yakiwemo magari 15 na baadhi ya silaha kutekwa.

Utawala wa kijeshi ambao umechukua madaraka baada ya mapinduzi ya Julai dhidi ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia umetangaza siku tatu za maombolezo.