1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHANGHAI: Rais Köhler akamalisha ziara ya China

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByA

Rais wa Ujerumani,Horst Köhler amemaliza ziara yake ya siku nne nchini China.Katika hotuba ya kuhitimisha ziara hiyo kwenye Chuo Kikuu cha Shanghai,Köhler alitoa mwito kwa China kushirikiana kupambana na tatizo la kubadilika kwa hali ya hewa duniani.Kwa mara nyigine tena alitoa wito wa kuhifadhi haki za binadamu.