1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHARM EL SHEIKH:Abbas na Olmert kukutana nchini Misri

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoT

Mkutano wa pande mbili baina kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert unatarajiwa kuanza katika mji wa pwani wa Sharm el Sheikh nchini Misri.

Mkutano huo unaazimia kutafuta njia za kuanzisha uhusiano mpya kati ya Palestina na Israel baada ya chama cha Fatah kinacho ongozwa na rais Mahmoud Abbas kujitenga na chama cha Hamas tangu chama hicho kilipoudhibiti Ukanda wa Gaza.

Hapo jana serikali ya Israel iliamua kuachilia mamilioni ya dola kwa utawala wa rais Mahmoud Abbas lakini maafisa wameeleza kuwa Israel bado inasita kuondosha vizuizi na vikwazo vinginevyo katika Ukingo wa Magharibi hadi pale utawala wa rais Mahmoud Abbas utakapo wajibika zaidi katika kupambana na wapiganaji wenye msimamo mkali.

Mazungumzo hayo yanahudhuriwa na rais Hosni Mubarak wa Misri na mfalme Abdullah wa Jordan.