1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHARM EL SHEIKH:Irak yafutiwa madeni na jumuiya ya kimataifa

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4v

Zaidi ya nchi 50 zimekubaliana na pendekezo la jumuiya ya kimataifa kusaidia kuimarisha hali nchini Irak.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano wa kimataifa juu ya Irak, unaofanyika katika pwani ya Sharm el Sheikh nchini Misri.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni pamoja na kuifutia Irak deni la dola zipatazo billioni 30, pamoja na ahadi za kusaidia ujenzi upya wa miradi mbalimbali nchini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moo ambaye ndiye mwenyekiti wa mkutano huo, alisema kuwa jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuisadia Irak.

Pembezoni mwa mkutano huo, Waziri wa Mmabo ya Nje wa Marekani, Condoleza Rice alifanya mazungumzo na mwenziye wa Syria Walid al Moualem.

Bi condoleza Rice leo hii anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Manouchehr Mottaki, pembezoni mwa mkutano huo.