1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shein ayafungua Maonyesho ya Muziki Würzburg

Admin.WagnerD5 Juni 2015

Tamasha la 27 la Kimataifa la Muziki wa Afrika limeanza mjini Würzburg nchini Ujerumani. Tamasha hili ambalo linalohudhuriwa pia vikundi vya sanaa kutoka visiwani Zanzibar litafikia tamati Juni 7.

https://p.dw.com/p/1FcHA
Deutschland 27. Africa Festival Würzburg
Picha: DW/S. Mnette

Rais wa Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein ni miongoni mwa maelfu ya watu kutoka pembe mbali mbali za dunia wanaohudhuruia Tamasha la kimataifa la siku nne la muziki wa Afrika mjini Würzburg hapa Ujerumani. Sudi Mnette ambaye yupo katika tamasha hilo la 27 lililoanza rasmi siku ya Alhamisi (04.06.2015) alizungumza na Dokta Shein akiwa mgeni rasmi na kwanza alimuuliza: Zanzibar kupewa kipaumbele zaidi katika tamasha hilo kubwa barani Ulaya kuna maanisha nini?

Kusikiliza mahojiano bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mahojiano:Mnette/Dk Shein

Mhariri:Josephat Charo