1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sherehe za krismasi.

Abdu Said Mtullya25 Desemba 2008

Baba Mtakatifu aongoza sherehe za krismasi.

https://p.dw.com/p/GMjI
Baba Mtakatifu Benedikt wa 16.

ROME:

Sherehe za kuadhimisha krismasi zimeanza duniani kote.

Baba  mtakatifu Benedikt wa 16 ,kama desturi aliongoza sala jana usiku.

Hapo  awali alijitokeza dirishani kwenye uwanja wa mtakatifu Petro na kuwasha mshumaa kama ishara ya amani.Katika ujumbe wake baba mtakatifu ametoa mwito juu ya  kukomesha   chuki na umwagaji damu katika mashariki  ya kati.

Na Katika mji wa Bethlehem,  kwenye ukingo wa magharibi, mamia ya watu walijipanga foleni ili kusali katika kanisa la uzawa  wa Yesu Kristo.

Kwa mujibu  wa historia ya dini ya ukristo,Bethlehem ndiyo mji ambako Yesu Kristo alizaliwa.