1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sherehe za Muungano wa Ujerumani zimeanza

Sekione Kitojo3 Oktoba 2010

Sherehe zimeanza nchini Ujerumani kuadhimisha miaka 20 tangu nchi mbili za Ujerumani zilipoungana tena ambapo sherehe zitafanyika rasmi mjini Bremen.

https://p.dw.com/p/PT5f
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kutoa hotuba wakati wa sherehe za miaka 20 za muungano wa Ujerumani mjini Bremen leo Jumapili.Picha: AP

Sherehe zimeanza nchini Ujerumani kuadhimisha miaka 20 tangu pale nchi mbili za Ujerumani zilipoungana tena, ambapo kutakuwa na sherehe katika mitaa mbali mbali pamoja na matamasha ya muziki katika mji mkuu Berlin, Bremen na kwingineko. Tarehe 3 Oktoba , 1990 Ujerumani iliungana tena rasmi baada ya miongo minne ya mtengano. Ukuta wa Berlin ulianguka kiasi miezi 11 kabla wakati Wajerumani waliposherehekea muungano wao mbele ya bunge mjini Berlin. Oktoba 3 ni siku ya mapumziko tangu wakati huo. Mwaka huu mji ambao una hadhi ya jimbo Bremen unakuwa mji utakaofanyika rasmi sherehe hizo. Maafisa wa mji huo wameweka mfano wa ukuta uliokuwa unatenganisha mji wa Berlin katika eneo la soko kuu, kuonyesha historia ya kugawika kwa nchi hiyo pamoja na picha za muungano pamoja na maandishi. Katika mkesha wa sherehe za leo Jumapili kansela Angela Merkel amesema kuwa ameshangazwa na jinsi Ujerumani mbili zilivyoweza kuungana kwa haraka. Anatarajiwa kuhutubia mjini Bremen leo Jumapili.