1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria mpya kwa wahamiaji nchini Ujerumani

Sekione Kitojo19 Oktoba 2010

Wahamiaji nchini Ujerumani watalazimika kusoma Kijerumani

https://p.dw.com/p/PhFr
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa na kundi la vijana kutoka familia za wahamiaji nchini Ujerumani.Picha: AP

Serikali  ya  kansela  Angela  Merkel  inatayarisha   sheria mpya  ambayo  itawataka  wahamiaji  kujijumuisha  vizuri zaidi  katika  jamii  ya  Ujerumani. Msemaji  wa   serikali amesema  mjini  Berlin  jana   kuwa   mapendekezo  hayo ni  pamoja  na  ulazima  wa   kusoma  lugha  ya  Kijerumani na  mtu anaweza kuadhibiwa ,iwapo  atashindwa   kumaliza  masomo yanayotakiwa  kwa  ajili  ya  kujumuishwa. Matokeo   kwa mtu  atakayeshindwa  inaweza  kuwa  pamoja  na kupunguziwa  mafao  ya  kijamii  ama   kubatilisha   ruhsa ya  kuishi  nchini. Hata  hivyo , muswada  huo , ambao unatarajiwa   kupigiwa  kura  mwezi  Desemba , pia utaimarisha   hatua  ya  kutambua  shahada  zilizopatikana kutoka  mataifa  ya  kigeni. Kiasi  cha wahamiaji wanaokadiriwa  kufikia  300,000  wanaoishi  nchini Ujerumani  kwa  hivi  sasa   wanashindwa  kufanyakazi walizojifunza   kwasababu  masomo  waliojifunza hayajathibitishwa  na  maafisa  wa  Ujerumani.