1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria tata ya uzalendo yaanza kutumika Zimbabwe

15 Julai 2023

Zimbabwe imeanza kutumia sheria inayotishia uhuru wa kujieleza ikiwa ni karibu mwezi mmoja kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini humo. Rais Emmerson Mnangagwa jana alitia saini kuanza kutumika kwa sheria hiyo.

https://p.dw.com/p/4TwdL
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
Rais wa Zimbabwe Emmerson MnangagwaPicha: Jekesai Njikizana/AFP/Getty Images

Sheria hiyo iliyopitishwa na bunge mwezi mmoja uliopita inataja kile kilichoitwa kuwa "kuumiza kwa makusudi uhuru na maslahi ya Zimbabwe" kuwa uhalifu, imekosolewa na vyama vya upinzani vikisema kuwa hiyo ni njia ya kukabiliana navyo kabla ya uchaguzi huo wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika Agosti 23.

Soma zaidi: Upinzani Zimbabwe waenda mahakamani baada ya zuio la mkutano

Chini ya sheria hiyo kwa mfano, mtu anayeunga mkono vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe anaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela au hata adhabu ya kifo ikiwa uhalifu umeainishwa kama uhaini mkubwa.

Wakosoaji wanasema sheria hiyo imeandikwa kwa njia isiyoeleweka kiasi kwamba raia yeyote anayeikosoa serikali anaweza kufunguliwa mashtaka.