1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shinawatra kurudi Thailand karibuni

25 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/Cg4c

BANGKOK

Waziri mkuu wa zamani wa Thailand aliyeko uhamishoni Thaksin Shinawatra amewaambia waandishi habari mjini Hongkong kwamba anatarajia kurudi Thailand katika muda wa wiki kadhaa zijazo.Hii ni baada ya ushindi wa chama chake cha katika uchaguzi ulifanyika mwishoni mwa juma.

Hata hivyo amesema atarudi nchini mwake kama raia wa kawaida tu na wala sio mwanasiasa.Thaksin aliondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Septemba mwaka jana na anatuhumiwa kwa kuhusika na ulaji rushwa.

Aidha Thaksin hajaondoa uwezekano wa kuwa mshauri mkuu wa chama cha Peoples Power Party kilichoshinda wingi mkubwa wa viti bungeni katika uchaguzi uliofanyika jumapili iliyopita.Chama hicho sasa kinajishughulisha na harakati za kuunda serikali ya mseto.