1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la Coach e.V latunukiwa zawadi

Oummilkheir27 Novemba 2007

Shirika linalowahudumia vijana wenye asili ya kigeni bwatuzwa zawadi ya Freiherr-vom Stein

https://p.dw.com/p/CTp8

Muasisi wa mpango wa kujumuishwa wageni uliopewa jina “Coach”-Mustafa Bayram ametunukiwa zawadi ya Freiherr-vom-Stein ya wakfu wa Alfred-Toepfer.Ametunukiwa zawadi hiyo yenye thamani ya yuro 25 elfu kwa mpango wake unaosifiwa wa kufungua kituo cha mafunzo na ushauri kwaajili ya vijana wenye asili ya kigeni.Kivutio kikubwa zaidi cha mpango huo ulioanzishwa miaka mitatu iliyopita ni ile hali ya kujumuishwa wazee katika shughuli za kuwaelemisha watoto wao.Wakfu wa Alfred-Toepfer unajitahidi pawepo umoja barani Ulaya kwa kuhifadhiwa tamaduni tifauti zilizoko na kuleta hali ya kuelewana kati ya wakaazi wa Ulaya.

Si rahisi kuipata ofisi hiyo iliyoko katika mtaa wa Cologne-Ehrenfeld- Oskar-Jäger-Strasse ,nyumba nambari 139.Iko nyuma ya uwa kati ya ghala moja na duka la zana za elektronik.Huko ndiko inakokutikana ofisi ya “Coach e.V”-mpango wa mafunzo na juhudi za kuwajumuisha katika maisha ya jamii vijana wenye asili ya kigeni.Kwa sasa kuna vijana 200 ndani ya ukumbi wa jingo hilo.

Wengi wao wamejiunga na mradi huo kwasababu wanakumbwa na shida shuleni,maki zao si nzuri,hawana hamu ya kwenda shule na matarajio yao pia si mazuri.Ndio maana shirika la Coach” limepania kuwasaidia ili waweze kujiendeleza vyema shuleni na akwa namna hiyo wawe na matumaini mema ya siku za mbele-anasema muasisi wa shirika hilo Mustafa Bayram:

“Lengo ni kuwawezesha wanafunzi wote wafanye vyema shuleni,wapasi mitihani yao na waweze kupaqta nafasiu ya kujifunza kazi.Tunajaribu kuhakikisha vijana wanajumuika ipasavyo katika maisha ya jamii,inamaanisha wanapata nafasi ya kujifunza kazi au wanajiunga na shule za sekondari na kuendelea.”

Shirika la Coach e.V linasaidia pia kutoa mafunzo ya lugha,na mafunzo mengineyo kwa wanafunzi wenye shida.Kuanzia kijerumani,kupitia hesabu na kiengereza hadi historia na kemia-orodha ya mafunmzo ni ndefu tuu na yeyore mwenye shida kati ya vijana hao,anasaidiwa-Misaada yote hiyo inatolewa na wataalam na kwa lugha ya kijerumani.Wakati huo huo lakini vijana wanajifunza jinsi ya kusoma ili kuinua uwezo wao.

Vijana hao wanasimulia kila mmoja jinsi wanavyoziangalia shughuli za shirika la Coach.

Toulma anasema huu ni msaada mkubwa kama mtu hakuelewa shuleni anaweza wakati wowote kuulitza na kufahamishwa.Na halai ni ya kuvutia kwasababu kuna marafiki huku.

Djalna Musule anasema amejiunga na Coach eV tangu miaka miwili iliyopita.Anakuja kila siku mara tatu au nne kwa wiki kwasababu ya matatizo shuleni na ghuku anasaidiwa,anaweza kujieleza na anasema anajisikia vizuri tuu anapokuwa na wenzake wa shirika la Coach e.V.

Kujumuika ipasavyo katika jamii inamaanisha kuwajibika nakuheshimiana.Muasisi wa shirikaq hilo Mustafa Bayram anasema wanazungumzia juu ya masuala chunguzima ikiwa ni pamoja na jinsi ya kueopukana na matumizi ya nguvu,na jinsi ya kujiepusha na mizozo.Kmsingi mada zote wanazokabiliana nazo vijana hujadiliwa kwa kina ili kuwawezesha vijana wawe na mtazamo mwengine kabisa wanapokabiliana na mizozo.

Kauli mbiu ya shirika la Coach e.V ni “urafiki miongoni mwa jamii.”

Shirika la Coach e.V linawakaribisha vijana wengine pia jaapo kama hawana asili ya kituruki.Mfano Ronie Ciplek anaetoklea Poland.

Mbali na kuwajumuisha wataalam kutoka nje mfano waalimu,wataalam wa huduma za jamii,shirika la Voach e.V linawajumuisha pia wazee katika shughuli zake.Mikutano ya wazee inaitishwa kila kwa mara ili kuwaarifu jinsi watoto wao wanavyoendelea.