1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la fedha Ulimwenguni lihayi

21 Aprili 2009

IMF ilidhaniwa inakufa na sasa imefufuka ?

https://p.dw.com/p/HbSE

Shirika la fedha Ulimwenguni (IMF) kwa miaka mingi likionekana linapoteza m aana yake na laiti mawazo kama hayo yamngeselelea, basi kubaki kwa shirika hilo kungehatarika.Kwa kadiri ulimwengu hivi sasa umekumbwa na msukosuko wa fedha na wa kiuchumi, shirika hili kutokana na uwezo wake wa kutoa mikopo limerudi kuhitajika zaidi.Nchi zenye upungufu wa fedha katika hazina zao,huligeukia shirika hilo la fedha Ulimwenguni kwa kiinua-mgongo.

Shirika la fedha Ulimwenguni (IMF) limerudi katika biashara yake ya kutoa mikopo.Hivyo ndivyo asemavyo waziri wa zamani wa fedha wa Ufaransa Dominique Strauss-Kahn .katika wimbi la sasa la msukosuko wa kiuchumi tayari dala bilioni 100 zimeshatolewa na shirika hilo kama mikopo kwa nchi zilizokumbwa na matatizo ya fedha .

Miongoni mwa nchi za kwanza kupokea mikopo hiyo, ni Iceland ,ambayo hazina yake imekauka na uchumi wake umekaribia kuporomoka kabisa.Mexico imepatiwa kitita cha dala bilioni 47 na hicho ndicho kima kikubwa kabisa kutolewa kw nchi yoyote hadi sasa.Baada ya Mexico zinafuata nchi kama Bellorusia,Lithuania,Hungary,Pakistna,Serbia na Ukraine.Lakini, nchi nyengine kama vile Uturuki,Rumania na Mongolia zimetoa maombi yao ya kusaidiwa na IMF-shirika la fedha ulimwenguni.Nchi nyengine zaidi zitafuata kupiga hodi mlangoni mwa IMF.

Dawa lakini, ya kuponesha maradhi ni chungu:

Shirika la Fedha ulimwenguni, lina akiba ya dala bilioni 250 na akiba ya tani 3,200 za dhahabu pamoja na kikosi kikubwa cha watumishi.Lakini ,hakuna aliepiga hodi mlangoni mwake mjini Washington kutaka mikopo pamoja na nasaha nini la kufanya.Kwani, dawa ambayo shirika hili lilokuwa likitoa kuponesha maradhi ya nchi zenye msukosuko ilikuwa chungu na kali mno.

Shirika hilo la Fedha likidai kama masharti ya mikopo yake kupunguzwa nakisi na fidia ,riba za juu na kupunguza matumizi ya kuwasaidia wanyonge.Katika baadhi ya nchi zilizofuata muongozo huo kulizuka uasi kwa njaa za masikini .

Katika sehemu kubwa ya nchi za Ulimwengu wa Tatu,shirika la fedha ulimwenguni likiangaliwsa kama fimbo ya nchi tajiri za kiviwanda .Nchi zinazoinukia kiuchumi kutokana na kustawi kwao kwa uchumi zilimudu kulikwepa shirika hilo la fedha ulimwenguni.katika kipindi cha cha mikopo rahisi hazikugeukia shirika hilo zinapokumbwa na shida ya fedha.Zilikopa fedha katika masoko ya fedha ulimwenguni tena kwa riba ndogo na bila ya kubidi kutekeleza masharti magumu ya IMF.Hata baadhi ya nchi zenye utajiri wa mali asili mfano wa Venezuela,hutoa mikopo na hivyo kushindana na shirika la Fedha ulimwenguni.Hii ikapelekea shirika hili kuanza kupoteza umaarufu wake na kuendewa panapozuka mahitaji.Kwani, mashauri yake linayotoa hayakutiwa mno maanani na hivyo likipungiwa na mapato ya riba kutokana na ukosefu wa mikopo ya kutoa.

Mageuzi sasa yanahitajika katika shirika hili:

Kutokana na kuongezwa akiba yake , nchi za Umoja wa Ulaya, zimelitia jeki kwa kima cha dala bilioni 100.China imechangia nayo dala bilioni 40.Brazil,ambayo miaka ya kwanza ya 1970 ilijikuta katika ukosefu wa fedha na mteja mkubwa wa IMF ,imechangia dala bilioni 4.5.Kwa ufupi, Shirika la fedha Ulimwenguni (IMF), limeibuka sasa ndilo lililofaidika mno na msukosuko wa sasa wa fedha duniani.

Mwansdishi:Karl Zawadzky-ZR/Ramadhan Ali

Mhariri:M.Abdul-rahman