1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la Msalaba Mwekundu Red Cross nchini Kenya wamo katika shughuli za kuwarejesha wakaazi makwao

5 Mei 2008

Nchini Kenya operesheni ya kitaifa ya kuwarejesha makwao wakaazi waliokuwa wakipewa hifadhi kwenye kambi za muda katika mkoa wa Bonde la Ufa imeanza rasmi hii leo.

https://p.dw.com/p/Dtwv
Watu waliokuwa wakiyahama makaazi yao baada ya ghasia za uchaguzi nchini KenyaPicha: AP

Taarifa zinaeleza kuwa kumeundwa vituo 32 vya polisi kwa lengo la kudumisha usalama katika eneo hilo. Hatua hii inachukuliwa baada ya Rais Mwai Kibaki na waziri Mkuu Raila Odinga wote wakiandamana na Makamu wa Rais kuzuru eneo hilo mwishoni mwa mwezi uliopita.Shughuli hiyo inayashirikisha mashirika ya msaada mfano Lile la Msalaba Mwekundu Redcross.

Thelma Mwadzaya alizungumza na Mkurugenzi wake Abbas Gullet ili kupata picha halisi