1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la Utangazaji la Zanzibar na haki za binaadamu

24 Juni 2011

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar, Hassan Mitawi, ameahidi kuwa shirika hili jipya litakuwa moja ya nyenzo za serikali kuimarisha hadhi na heshima kwa haki za binaadamu visiwani Zanzibar.

https://p.dw.com/p/RVgI
Andrea Schmidt (kulia) na Mohammed Abdul-Rahman (kushoto) wa Deutsche Welle wakizungumza na Hassan Mitawi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar, wakati Mitawi alipotembelea Deutsche Welle tarehe 22 Juni 2011.
Andrea Schmidt (kulia) na Mohammed Abdul-Rahman (kushoto) wa Deutsche Welle wakizungumza na Hassan Mitawi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar, wakati Mitawi alipotembelea Deutsche Welle tarehe 22 Juni 2011.Picha: DW

Mohammed Khelef anazungumza na Hassan Mitawi juu ya ushiriki wake kwenye kongamano la kimataifa la siku tatu la Deutsche Welle Global Media Forum, lililofanyika mjini Bonn, Ujerumani, kuanzia tárehe 20 hadi 22 Juni 2011.

Pamoja na mambo mengine, Mitawi anazungumzia dhima ya shirika jipya la utangazaji la Zanzibar (Zanzibar Broadcasting Corporation) katika masuala ya haki za binaadamu kupitia vyombo vya habari.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Hassan Mitawi
Mhariri: Othman Miraji