1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la WFP lagawa chakula jimboni Equatorial

Josephat Nyiro Charo4 Juni 2010

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR jumla ya wakimbizi laki moja na thelathini waliyakimbia mapigano baina ya wanajeshi na wapiganaji wa Enyele jimboni Equateur Novemba mwaka jana

https://p.dw.com/p/NiQt

Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, shirika la mpango wa chakula duniani WFP, limeanza kuwagawia chakula wakimbizi wa jimbo la Equateur lililoko eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Takriban watu alfu ishirini na mbili tayari wanapokea chakula cha msaada kinachotolewa na shirika la WFP kwa hisani ya Ufaransa, Uingereza na Ujerumani. .Taarifa kamili anazo mwandishi wetu wa Kinshasa Saleh Mwanamilongo.