1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shughuli za kulinda amani za umoja wa mataifa

Oumilkher Hamidou24 Januari 2009

Mwito wa mkuu wa tume za kulinda amani za Umoja wa mataifa

https://p.dw.com/p/GfLK

New-York:

 Tume 18 za kulinda amani za umoja wa mataifa,zilizoko katika kila pembe ya dunia zinajikuta ukingoni mwa kuelemewa-hayo ni kwa mujibu wa msimamizi wa shughuli za tume hizo za kimataifa.Kwa sasa kuna wanajeshi laki moja na 13 elfu,polisi na wasimamizi wa kiraia wanaotumikia shughuli za umoja wa mataifa kote ulimwenguni-anasema mkuu wa tume za kulinda amani za umoja wa mataifa Alain Le Roy mjini New-York.Hali hiyo inatishia zaidi shughuli za tume ya Umoja wa mataifa katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na katika jimbo la misuko suko la Darfour nchini Sudan-amesema Alain Le Roy.