1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria Cassava

Sekione Kitojo31 Desemba 2011

watafiti nchini Nigeria wamegundua aina tatu mpya za muhogo, ambazo wanasema zitasaidia kupambana na utapiamlo unaosababishwa na upungufu wa vitamini A.

https://p.dw.com/p/13cAk
Utapiamlo ni tatizo kubwa katika bara la Afrika.
Utapiamlo ni tatizo kubwa katika bara la Afrika.Picha: dapd

Wakitumia mbegu maalum za muhogo chotara, watafiti nchini Nigeria wamezalisha aina tatu mpya za muhogo zenye rangi ya njano , ambazo wanasema zitasaidia kupambana na utapiamlo unaosababishwa na upungufu wa vitamini A katika eneo hilo. Muhogo ni zao kuu la chakula katika sehemu kubwa ya bara la Afrika.

Lakini mafanikio ya utafiti huo yamekataliwa na kundi la marafiki wa dunia nchini Nigeria FoEN , ambalo limeliambia kundi la taasisi ya kimataifa ya kilimo katika maeneo ya joto mjini Ibadan kusitisha hatua ya kuchezea zao kuu la chakula nchini Nigeria, wakidai kuwa wanakwenda kinyume na uhai anuai.

Wanaharakati wa kundi hilo la mazingira pia wanasema kuwa caroti mbili zinaweza kirahisi kutoa mahitaji ya siku nzima ya vitamini A.

Mapema mwezi huu, taasisi ya IITA , ikifanyakazi pamoja na taasisi ya taifa ya utafiti wa mazao aina ya mihogo, ilitangaza mafanikio ya kuzalishwa kwa mmea wa muhogo ambao kiasili unaweza kutoa kiwango cha juu cha beta- carotini , ambayo ni kemikali ya asili inayohusika na rangi ya chungwa katika matunda na mboga.

Mwili unabadilisha kemikali hiyo ya beta- karotini kuwa vitamini A. Mboga kama karoti, brokoli na mchicha ni vyanzo vizuri vya beta - karotini, ambayo inasaidia katika kuzuwia baadhi ya saratani na kupunguza kasi ya kuenea kwa mtoto wa jicho, miongoni mwa faida nyingine za kiafya.

Muhogo ambao unakiwango kikubwa cha wanga , ukiwa ni mti unaokua kama kichaka ambao mizizi yake ni chakula, ni chakula kikuu cha tatu duniani baada ya ngano na mchele, na ni msingi mkuu wa lishe kwa zaidi ya watu milioni 600 katika mataifa ya ulimwengu wa nchi zinazoendelea.

Wastani wa matumizi ya muhogo nchini Nigeria kwa siku , taifa linalozalisha kwa wingi zao hilo katika bara la Afrika , ni gramu 600 kwa mtu mmoja . Lakini nchi hiyo inatarajia kuongeza uzalishaji maradufu kwa mwaka wa tani milioni 37 chini ya mpango huo wa mabadiliko ya uzalishaji , uliozinduliwa Agosti mwaka 2011 kuimarisha thamani iliyoongezwa kupitia uzalishaji unaotegemea mahitaji pamoja na mavuno yaliyoongezeka.

Peter Kulakow , mzalishaji wa mimea na mtaalamu wa vinasaba katika taasisi ya IITA nchini Nigeria , amesema kuwa baada ya miaka 20 ya utafiti , hii ni mara ya kwanza kwamba aina za muhogo zikiwa na beta-karotini ya kutosha , ambayo pia inajulikana kama vitamini A, ambayo itaondoa tatizo kubwa la mahitaji ya kiafya ya lishe , imepatikana katika bara la Afrika.

Aina mpya tatu hazijapatiwa hati za umiliki kwa kuwa zinaonekana kuwa ni kitu kizuri kwa dunia katika kupunguza njaa na umasikini.

Kulakow, kiongozi wa uzalishaji wa mimea ya muhogo katika taasisi ya IITA, ameliambia shirika la habari la IPS njaa iliyojificha inayosababishwa na ukosefu wa vitamini A, ni tatizo kubwa ambalo halijatatuliwa katika hatua endelevu kwa kutumia njia nyingine, hususan kwa wanawake na watoto,

Mwandishi: Sekione Kitojo / IPS

Mhariri : Caro Robi