SI MUSTAFA.Kundi la Islamic Maghreb limekiri kufanya mashambulio ya mabomu
14 Februari 2007Matangazo
Kundi la Islamic Maghreb linaloshirikiana na kundi la kigaidi la Al Qaeda limekiri kuhusika na mashambulio ya mabomu ya hivi karibuni nchini Algeria.
Watu sita waliuwawa na wengine 30 walijeruhiwa katika mfululizo wa mabomu saba yaliyolipuka mapema jana katika eneo la mashariki mwa mji mkuu wa Algiers.