1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SIDMOUTH : Meli yamwaga mafuta baharini

22 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYx

Tani 3,500 za mafuta kwenye meli ya mizigo ya Uingereza iliopwelezwa mchangani kwenye mwambao wa kusini mashariki ya Uingereza kimekuwa chanzo cha wasi wasi mkubwa kwa walinzi wa mwambao wanaotarajia kuepusha maafa ya kimazingira ya muda mrefu.

Pual Coley msemaji wa walinzi wa mwambao amesema wataanza kusafisha tani 200 au zaidi za mafuta yaliovuja baharini mapema leo asubuhi.

Meli hiyo MSC Napoli iliopata matatizo kutokana na kuchafuka kwa bahari inabeba makontena 2,323 ya betri za acid, mafuta mazuri, vipuri vya mgari na baadhi ya vitu vinavyotajwa kuwa vya hatari ikiwa ni pamoja na kemikali za viwandani na kilimo.

Baadhi ya makontena yamesombwa na maji.

Meli hiyo ilipwelezwa mchangani na matishali hapo Jumamosi katika juhudi za kuizuwiya isizame na wafanyakazi wake 26 waliondolewa kwenye meli hiyo na helikopta za uokozi za wanamaji wa Uingereza.