1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sierra Leone kuendelea na mechi yake ya AFCON

1 Septemba 2014

Kutokana na kitisho cha Ebola, Sierra Leone imelazimika kuwatumia wachezaji wote wanaocheza soka lao nje ya nchi hiyo katika mechi za kufuzu katika dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika.

https://p.dw.com/p/1D4tM
Fußballnationalmannschaft Sierra Leone
Picha: FETHI BELAID/AFP/Getty Images

Serikali nyingi za Afrika zimeweka hatua za kujikinga na nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia ambazo zimeathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo uliowauwa watu 1,552 kufikia sasa.

CAF ilizitaka nchi zilizoathirika yaani Guinea na Sierra Leone zihamishe mechi zake ili kupunguza kitisho cha kusambaa virusi hivyo na kama anavyoeleza msemaji wa shirikisho hilola soka Erick Mwanza, hatua hiyo siyo adhabu bali tahadhari. Anasema CAF inashirikiana na wadau wote wa kandanda kuhakikisha kuwa wanashirikiana katika kipunguza kitisho cha kueneea mlipuko huo wa Ebola

Shirikisho la Soka nchini Sierra Leone linasema linapanga kuendelea na mechi yake ya kwanza katika Kundi D dhidi ya Cote d'Ivoire mnamo Septemba 6 mjini Abidjan lakini itawatumia wachezaji wake 20 wanaocheza katika mataifa ya ng'ambo.

Serikali ya Cote d'Ivoire ilisema kuwa haitaruhusu mechi hiyo kuchezwa mjini Abidjan na Shirikisho la soka nchini humo halikuwa limetangaza nchi iliyo tayari kuuandaa mchuano huo. Sierra Leone kisha ilistahili kuelekea mjini Accra, Ghana, kucheza dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mnamo Septemba 10. Mahali pa mchezo huo pamebadilishwa na sasa utachezwa katika mji mkuu wa pili nchini Kongo, Lubumbashi. Guinea inatarajiwa kucheza mechi yake mnamo Septemba 6 dhidi ya Togo mjini Casablanca, Morocco.

Mwandishi; Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Saumu