1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku 100 za serikali ya Ujerumani

Sekione Kitojo
21 Juni 2018

Siku 100 za serikali ya mseto Ujerumani, kikao maalum kati ya Merkel na Umoja wa Ulaya cha sera za uhamiaji,na kujitoa Marekani katika baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ni mada katika magazeti ya Ujerumani. 

https://p.dw.com/p/300NR
Gedenktag für die Opfer von Flucht und Vertreibung mit Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und Horst Seehofer (CSU), Bundesminister des Innern, für Bau und Heimat
Kansela Angela Merkel (kushoto) pamoja na kiongozi wa chama cha CSU Horst SeehoferPicha: picture-alliance/dpa/K.Nietfeld

Tukianza  na  gazeti  la Manheimer Morgen,  mhariri  anaandika kuhusu  siku  100  tangu  kuingia  madarakani serikali  ya  muungano nchini  Ujerumani. Mhariri  anaandika:

"Kansela Angela  Merkel  na  chama  chake  atapungukiwa  na  viti viwili  tu  bungeni  iwapo chama ndugu  cha  CSU  kitajitoa katika muungano  unaounda  serikali.  Hatua  kama  hiyo  itakuwa ni mapinduzi  makubwa  kwa  kipindi  chote  cha  bunge kilichobakia.

Kwa  kuwa  katika  wowote  ule Ujerumani  inapaswa  kwa  kiasi fulani  kupumua  baada  ya  mwaka  mmoja wa  viongozi kudhoofisha. Kile  kinachosababisha  wasi  wasi, ni  kwamba  mbali na  chama  cha  Kijani, ambacho  wakati  ule kilionekana  kuwa katika  nafasi  ya  kimkakati, vyama  vyote  vingine  vilikuwa vinajitathmini, kuhusiana  na fursa ndogo walizonazo  wakati  huo ama  baadaye."

Mhariri  wa  Gazeti  la  Weser-Kurier  la  mjini  Bremen,  akiandika kuhusu  siku 100  za  serikali  ya  muungano  ya  Ujerumani anasema, kitisho  cha  chama  cha  CSU  kujitoa  katika ushirika  na chama  cha   kansela  Angela  Merkel  cha  CDU  hatimaye kimekwisha. Mhariri  anaendelea:

"Hali  hiyo  inavutia  kwa  kila  upande. Lakini  chama  cha  CSU hakitaki kuikumbatia  hali  hiyo. Chama  hicho  kinataka  kuendelea kufuata  mkakati wake, kama  ambavyo  viongozi  wa  chama  hicho Horst Seehofer  na Markus Soeder  walivyojipanga.  Kitisho  cha kuvunja umoja wa vyama  hivyo  ni  makelele ya  bure. Kujitoa  katika kushiriki  katika  serikali , kutakuwa  na  maana  tu  ya  kuweka haki ya  kiliberali  ya  waombaji  hifadhi  kupitia  chama  cha  Kijani. Kila la  kheri  katika  uchaguzi  wa  jimbo  la  Bavaria, na  kwa  ukweli muda  unayoyoma  sio  kwa  Merkel , lakini  kwa  chama  cha  CSU. Chama  hicho  kinapaswa  hadi  Juni 30  kupata  jibu  mjarabu, kwanini  kiendelee  kufuata  njia  ya  kansela, wakati  binafsi hakiwezi  kupata  jibu  linalostahili  kutoka  katika  mkutano wa Umoja  wa  Ulaya."

Kuhusiana  na  mkutano  maalum  kati  ya  kansela  Merkel  na Umoja  wa  Ulaya  kuhusu sera  za  kuomba  hifadhi  katika  mataifa ya  Umoja  huo, mhariri  wa  gazeti  la Neue Osnabrueker Zeitung anaandika.

"Katika  Umoja  wa  Ulaya, anayetaka  kuidhinisha  kitu , ni  lazima kimsingi amsaidie mwingine. Hali  hii  anaifahamu  bila  shaka kansela  Merkel  kuliko  mtu  mwingine  yeyote. Anafahamu  kwamba kupata  kuungwa  mkono  na  mataifa  mengine  ya  Umoja  wa Ulaya  katika  mzozo wa  wahamiaji  katika  mkutano  maalum  ni lazima  kutoa  chochote.  Hiyo  ni  nafasi  kwa  serikali  nyingine  za Umoja  wa  Ulaya, kuweka  sawa  mambo  mengine  ya  zamani.  Bila shaka  nchi kama  Ugiriki  yenye  madeni mpaka  puani, ambayo mpango wake  wa  msaada  unafikia  mwisho  mwezi Agosti, itataka kwa  njia  moja  au  nyingine  Ujerumani itoe  msaada. Hii  ina maana wakimbizi  kwa  unafuu wa  madeni ? Ama wakimbizi  kwa bajeti  ya  eneo  la  sarafu  ya  euro, kama  inavyotaka  Ufaransa ? Merkel  anajitumbukiza  katika  mkanganyiko mwenyewe,  ambao kujitoa  itamlazimu  kutumia  fedha, na  itakuwa   kuwabebesha mzigo  walipa  kodi  wa  Ujerumani."

Gazeti la Frankfurt Rundschau likiandika  kuhusu  kujitoa  kwa Marekani  katika  baraza  la  Umoja  wa  mataifa  la  haki  za binadamu, mhariri  anaandika.

"Kujitoa  kwa  Marekani  hakutakuwa  na  athari  zozote, na  pia  hali ya  haki  za  binadamu  haitakuwa  bora   zaidi. Baraza  hilo  ni  mara chache  linapata  haraka  suluhisho  katika  suala  hilo. Mjadala utakaoendelea  kuwapo unachangia  katika  diplomasia , na  mfano ni  kuhusu mpango  wa  kinyuklia  wa  Iran  unaothibitisha  kuhusu majadiliano  ambayo  hayaleti  tija."

Ni  maoni  ya  wahariri  wa  magazeti  ya  Ujerumani  kama yalivyokusanywa  na  Sekione  Kitojo.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Iddi Ssessanga