1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku mbili za mapigano zasababisha mauaji ya watu 81 Mogadishu

21 Aprili 2008

hali bado ni mbaya Somalia ambako hakuna serikali madhubuti

https://p.dw.com/p/DlMU

MOGADISHU

Kundi maarufu la kutetea haki za binadamu nchini Somalia Elman limefahamisha kwamba katika siku mbili za mapigano yaliyozuka upya kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu watu 81 waliuwawa na wengine wengi wakajeruhiwa.Waandishi wa habari nchini humo wamearifu kuwa wanajeshi wa serikali ya mpito wakiungwa mkono na wanajeshi wa Ethiopia walipambana vikali kwenye mapigano ya jumapili ambapo makombora yalitumika katika mashambulio na kiasi cha watu 29 wakauwawa.Somalia imekumbwa na machafuko tangu wanajeshi wa Ethiopia walipoingia nchini humo na kuwafurusha wafuasi wa mahakama za kiislamu waliokuwa wakidhibiti maeneo mengi ya Somalia.Ghasia hizi mpya zimesababishwa na jaribio la kutaka kuwatimua wanaharakati wa mahakama za kiislamu katika mji wa Huriwa kaskazini mwa mji wa Mogadishu.Taarifa nyingine zinasema kwamba boti la uvuvi la hispania likiwa na wafanyikazi 26 limetekwa nyara na maharamia wa Somalia na hatma ya watu hao haijajulikana.