1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya akinamama ulimwenguni

8 Machi 2011

Akinamama waadhimisha miaka 100 tangu walipoanzisha juhudi za kudai haki sawa na wenzao wa kiume.Jee juhudi hizo zimeleta matunda yanayotarajiwa?

https://p.dw.com/p/10V9x
Wanafunzi waadhimisha siku ya akinamamaPicha: picture alliance/dpa

Siku ya wanawake ulimwenguni imeanza kuadhimishwa tangu miaka 100 iliyopita nchini Denmark,Ujerumani,Austria,Uswisi,Bulgaria na Marekani. Wakati ule akinamama zaidi ya milioni moja waliteremka majiani kudai haki yao ya kimsingi- haki ya kupiga kura.

Hebu fikiria, miaka mia moja iliyopita wanawake hawakuwa hata na haki ya kupiga kura katika nchi nyingi za dunia. Hii leo, siku ya akinamama inaadhimishwa kwa kutathmini maendeleo yaliyoweza kupatikana tangu wakati huo, na kuzingatia changamoto zinazowakabili wanawake katika kila pembe ya dunia.

Nchini Ujerumani siku ya akinamama iliyopewa jina na mtandao wa akinamama wa Berlin- "Miaka mia moja ya subira- miaka 100 ya ghadhabu" inaadhimishwa kwa namna mbali mbali. Licha ya baadhi ya ufanisi, bado hali inadhibitiwa na wanaume- na hasa linapohusika suala la ajira, wanalalamika wanamtandao. Idadi kubwa zaidi ya akinamama katika daraja za uongozi ikilazimika itengwe idadi na kuwarahisishia akinamama njia za kuweza kufungamanisha kazi na familia. Hilo ni dai la mawaziri wa kike wa serikali kuu.

Bibi Jutta Wagner, mwenyekiti wa shirikisho la wanasheria wa Ujerumani, anahisi maendeleo yaliyofikiwa ni haba:

NO FLASH 100 Jahre internationaler Frauentag 2011
Haki sawa kwa wotePicha: picture alliance/dpa

"Maendeleo ni haba mno kuweza kusema kwamba pengine mwaka 2090 idadi kubwa zaidi ya wakinamama watakauwa wanashikilia nyadhifa za juu za uongozi". Hali hiyo, itabadilika tu ikiwa kweli sheria maalum zitatumika- hivyo ndivyo tunavyoamini hasa kutokana na uchunguzi tulioufanya- imani yetu ni kubwa kuliko wakati wowote ule mwengine.

Marekani siku ya kimataifa ya akinamama inapita bila ya harakati zozote zile, licha ya kwamba bunge limeitambua rasmi siku hiyo tangu mwaka 1994. Hata hivyo, dai kuu la vuguvugu la akinamama nchini humo ni kuona kifungu kinachohusiana na haki sawa kati ya jinsia kinaingizwa katika katiba.

Katika ulimwengu wa kiarabu haijulikani bado kama wimbi la mageuzi linalopiga hivi sasa litabadilisha pia hali ya akinamama katika nchi hizo. Katika wakati ambapo nchini Syria akinamama wanaruhusiwa kufanya kazi bega kwa bega na wenzao wa kiume, nchini Saudi Arabia, kwa mfano, ndio kwanza akinamama wanadai haki ya kuruhusiwa kuendesha gari.

NO FLASH 100 Jahre internationaler Frauentag 2011
Mauwa kwa wakainamamaPicha: photlook/Fotolia

Barani Afrika, tunachukua mfano wa Kenya, ambako ingawa siku ya kimataifa ya akinamama si siku ya mapumziko, hata hivyo, jumuiya ya wanawake na maendeleo-jumuiya kubwa yenye wanachama zaidi ya milioni nne na nusu, inawazindua akinamama mnamo siku hii ya leo wawajibike zaidi, hasa kwa kuzingatia uchaguzi wa mwakani pamoja na kushadidia mshikamano pamoja na dada zao katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Mwandishi:ZPR/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Miraji Othman