1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kimataifa ya Amani

21 Septemba 2012

Leo ni siku ya kimataifa ya Amani, na shughuli mbali mbali zinafanyika katika sehemu nyingi za dunia kujadili suala la amani na usalama.

https://p.dw.com/p/16CFq
Wanawake barani Afrika wakabiliwa na athari kubwa ya kukosekana kwa amani
Wanawake barani Afrika wakabiliwa na athari kubwa ya kukosekana kwa amaniPicha: Babou Diallo

Huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanawake wameketi kutafakari masaibu wanayoyapata kutokana na kukosekana kwa amani katika eneo lao, na nchini Togo, maelfu ya wanawake wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo, wakitaka sauti zaidi katika maamuzi yanayohusu usalama wao. Kutaka kujua hali ya akina mama kiusalama kwenye siku ya leo, Daniel Gakuba mezungumza na Rukia Subow, mwenyekiti wa shirika la maendeleo ya akina mama nchini Kenya, na ameanza kwa kuzungumzia madhara ya vita kwa wanawake.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri:Miraji Othman