1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kupambana na Malaria duniani

Saumu Mwasimba25 Aprili 2009

Vita dhidi ya malaria barani Africa bado ni Tatizo

https://p.dw.com/p/He0R
Dawa ya kunyunyiza ya DDT, hutumika zaidi barani afrika kuua mbu wanaosababisha MalariaPicha: picture-alliance/dpa

Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na shughuli za kuwahudumia watoto UNICEF limesema kwamba kila sekunde 30 duniani mtoto mmoja anakufa kutokana na maradhi ya Malaria.

Kwa mujibu wa shirika hilo juhudi za kukabiliana na Malaria ni lengo linalopewa kipaumbele na Umoja wa mataifa katika kufikia malengo ya maendeleo ya Millenium ya Umoja huo kufikia mwaka 2015.

Hata hivo pamoja na juhudi zinazochukuliwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo shirika la UNICEF limekadiria kwamba watu millioni moja hufariki kila mwaka kutokana na maradhi hayo.

Leo ni siku ya kupambana na Malaria duniani na kwa mujibu wa UNICEF vifo vingi vinavyotokana na ugonjwa huo vinatokea katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Africa ambapo zaidi ya wanaoathirika ni watoto walio chini ya umri wa miaka 5.Takriban akina mama wajawazito millioni 50 wako hatarini kupata Malaria kila mwaka.