1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kwanza ya ziara ya Merkel Algeria.

Walter Langlott17 Julai 2008

Katika ziara yake ya kwanza nchini Algeria kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefanya mazungumzo na viongozi wa taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

https://p.dw.com/p/Ee4u
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ,kushoto akizungumza na rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika mwanzoni mwa ziara ya kansela Merkel ya siku mbili nchini humo.Picha: AP



Katika ziara yake ya kwanza nchini Algeria, kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefanya mazungumzo na uongozi wa kisiasa wa taifa hilo la Afrika ya kaskazini. Mazungumzo yao yalihusu zaidi uhusiano wa kiuchumi, ambapo katika tathmini ya Merkel kuna nafasi kubwa ya kuendelezwa, lakini pia yalihusu mapambano dhidi ya ugaidi wa makundi ya Kiislamu.




Angela Merkel alilakiwa kwa gwaride la kijeshi na mwenyeji wake rais Abdelaziz Bouteflika ,wakati alipowasili katika uwanja wa ndege mjini Algiers na kupigiwa mizinga 21.

Heshima ambayo hupatiwa tu rais wa nchi. Pia lililowazi ni kuwa ziara hii ya mwanzo ya kansela ina maana gani. Kansela Merkel anasisitiza kuwa anataka kuimarisha uhusiano na nchi ya Algeria.

Katika mazungumzo yangu ya kwanza na rais na waziri mkuu amesema Merkel, nimeweka wazi, kuwa uhusiano huu unaweza kuimarishwa zaidi. Kuna utamaduni wa muda mrefu, katika utendaji wa pamoja katika masuala ya kiuchumi, na sio tu kwa utawala uliopita wa Ujerumani lakini pia hata kwa iliyokuwa serikali ya Ujerumani ya mashariki DDR. Huo ulikuwa wakati uliopita lakini kwa kiasi fulani uhusiano huo ulisinzia, na tunataka sasa kuurejesha katika hali yake. Tunataka kutumia nafasi yetu hii.

Na nimeweka mkazo ili tuufungue mlango.

Majadiliano yake pia yalituwama katika ushirikiano wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuiuzia nchi hiyo silaha na kutoa ombi la kulipa mafunzo jeshi la Algeria. Algeria inapata silaha zake nyingi kutoka Urusi lakini pia inavutwa na Ufaransa na Marekani kununua silaha kutoka huko. Pia katika masuala ya teknolojia hususan katika kujipatia nishati endelevu, Algeria imeonyesha kuvutiwa sana na Ujerumani. Merkel amesema kuwa kuna wafanyabiashara kutoka upande wa mashariki ya Ujerumani , kwa mfano katika masuala ya yamashine za kuzalisha nishati zinazotumia gesi na nishati ya jua, hili ndilo ambalo Algeria imekuwa ikivutiwa sana nalo. Gesi ya Algeria inaweza kutumika kwa muda wa miaka 40 hadi 50 kabla ya kumalizika. Wanafahamu kuwa ni lazima itamalizika na kwa hiyo kizazi kijacho kiwe na kitu cha kutumia. Asilimia 60 au zaidi ya watu nchini Algeria wako chini ya umri wa miaka 25, na wanahitaji nafasi, katika maisha yao ya baadae.

Kwa upande mwingine Ujerumani inavutiwa na masuala ya kiuchumi ambayo ni pamoja na mafuta na gesi ya ardhini kutoka Algeria. Ujerumani kwa sasa inaagiza kiasi cha asilimia 40 ya mahitaji yake ya gesi kutoka Urusi na ni asilimia moja tu inayoagiza kutoka Algeria. Nchi hizi mbili pia zinataka ushirikiano wa karibu kuhusiana na masuala ya nishati endelevu.




►◄