1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G20 kujadili suluhisho la mzozo wa Syria

Admin.WagnerD16 Novemba 2015

Kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa mjini Paris viongozi wa nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani wa kundi la G20wanaokutana nchini Uturuki wanatarajiwa kutafuta suluhisho la pamoja la kupambana na Ugaidi.

https://p.dw.com/p/1H6Ru
G-20-Gipfel in Antalya Obama und Putin
Viongozi wakiwa katika mkutano wa G20Picha: picture-alliance/AP Photo/S. Walsh

Ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya mkutano huwo wa kundi la G20 unaendelea mjini Antalya, Uturuki, mikutano kadhaa mengine ya pembezoni imepangwa kufanyika leo hii ili kujadili hatua za kuutatua mzozo wa Syria pamoja na kampeni za mauaji za kundi la IS.

Rais wa Urusi Vladimir Putin pamoja na Rais wa Uingereza David Cameron wanaotarajiwa kukutana kwa mazungumzo leo, wote wamesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za pamoja dhidi ya ugaidi kufuatia mashambulizi yaliyofanywa mjini Paris.

"Tuna tofauti zetu na Urusi, kwasababu wanadhalilisha makundi yasiyo IS, makundi yanayompinga Asaad, watu wanaoweza kuijenga Syria ya baadae. Lakini nitakalomwambia Vladimir Putin ni hili - kuna jambo moja tunaweza kukubaliana, tutakuwa na usalama Urusi na Uingereza kama tutalitokomeza kundi la IS. Hilo ndio jambo la kuzingatia," alisema David Cameron

Putin naye kwa upande wake amesema mahusiano baina ya Urusi na Uingereza kwa sasa sio mazuri, na kuongeza kwamba mataifa hayo mawili yanahitaji kukuza mahusiano yao siku za mbele.

G-20-Gipfel in Antalya David Cameron
Rais wa Uingereza David CameronPicha: picture-alliance/dpa/S. Guneev

Obama kukutana na viongozi wa Ulaya

Aidha rais wa Marekani Barack Obama atakutana na viongozi kadhaa wa nchi za Ulaya ikiwamo Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Italia. Hata hivyo Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, hakuhudhuria mkutano huwo na kubaki Ufaransa akikabiliana na yaliyofuatia baada ya mashambulizi hayo. Lakini waziri wa mambo ya nje, Laurent Fabius, atahudhuria mkutano huwo utakaoongozwa na Rais wa Marekani.

Obama pia alikutana na Putin jana - kiongozi mwenye umuhimu katika jitihada za kumaliza mzozo wa Syria uliotengeza mazingira ya kuibuka kundi la IS- mazungumzo yao yalidumu kwa nusu saa na walijadili hatua za kidiplomasi kuhusu suala la ugaidi. Siku hio hio Obama pia alikutana na Mfalme Salman wa Saudi Arabia, kiongozi mwengine muhimu katika kuumaliza mzozo wa Syria.

Hatua za kiuchumi ndani ya ajenda ya G20

Mbali na machafulo kadhaa yaliyougubika ulimwngu, ajenda ya mkutano wa mwaka huu wa kundi la G20 pia inajumuisha kujadili hatua za kukuza uchumi wa dunia. Jitihada za ziada zikielekezwa katika kukabiliana na athari za kiuchumi, zilizotokana na kushuka kwa uchumi wa China.

Katika rasimu ya mwisho ya kundi hilo la G20 iliyowafikia shirika la habari la AP, imeonesha kwamba viongozi hawo wamezingatia lengo la pamoja la kukuza pato la ndani la taifa kwa asilimi 2 ifikapo mwaka 2018.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/ape

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman