1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya siku yawadia Marekani

Oumilkher Hamidou20 Januari 2009

Wamarekani na ulimwengu kwa jumla wasubiri kwa hamu kuapishwa rais wa 44 wa Marekani-wa kwanza mwenye asili ya kiafrika

https://p.dw.com/p/GcXf
Rais mteule Barack Hussein ObamaPicha: AP


Wamarekani,weusi kwa weupe,na raia wengineo waliopania kushuhudia kwa macho yao tukio la kihistoria, wamejaa majiani mjini Washington,saa chache kabla ya rais wa kwanza mwenye asili ya kiafrika,Barack Hussein Obama kukabidhiwa hatamu za uongozi,kwa kua rais wa 44 wa dola hilo kuu la dunia.


Hata kabla ya sherehe zenyewe zinazotazamiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu milioni mbili,maelfu ya wamarekani wenye asili ya kiafrika wameteremka Washington ili kushuhudia kwa macho yao ndoto ya Martin Luther King ikigeuka kua ukweli wa mambo.


Familia kadhaa kutoka kila pembe ya Marekani zimejazana majiani na mitaani wakisubiri kwa hamu aapishwe rais waliempigia kura kwa wingi ,November nne mwaka jana.


Renita King,mkaazi wa Houston,kusini mwa Marekani anasema amekuja Washington,kwa niaba ya mamaake mwenye umri wa miaka 73."Asingeweza kamwe kuamini kama tukio kama tukio kama hili lingewezekana"-Amesema hayo bibi huyo mwenye umri wa miaka 46.

Wengi kati ya wamarekani wenye asili ya kiafrika,ambaso ni asili mia 14 yaa wakaazi jumla wa Marekani,wanahofia njama ya kutaka kumuuwa rais huyo wa 44,ambae ameshapokea vitisho kutoka makundi ya kibaguzi.

Hisia za kibaguzi bado zingalipo.Hata hivyo utafiti wa maoni ya umma uliochapishwa jana,siku ya kukumbuka siku aliyouliwa mwanaharakati wa haki za binaadam Martin Luther King, hisia za kibaguzi zimepungua nchini Marekani katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.


Katika mahojiano na gazeti la Washington Post, Barack Obama binafsi amesema anataambua umuhimu wa kuchaguliwa kwake kama rais kwa jamii ya wamarekani wenye asili ya kiafrika.


"Kizazi kizima kitakua kikiwa na ushahidi hatamu za uongozi nchini mwao zinashikiliwa na mtu mmarekani mwenye asili ya kiafrika.Ni mageuzi ya kina hayo.Yatashawishi mtazamo wa watoto weusi kuelekea mustakbal wa maisha yao wenyewe.Yatzabadilisha pia mtazamo nwa watoto weupe kuelekea wenzao wenye asili ya kiafrika."Na tusidharau kipeo cha hali hiyo."


Amesisitiza Barack Hussein Obama atakaeapishwa saa mbili na dakika moja kwa saa za Afrika Mashariki hii leo.Ataweka mkono wake juu ya biblia ile ile aliyoapishwa Abraham Lincoln,rais wa Marekani aliyepiga marufuku utumwa.


Barack Obama anasema wataanza kuijenga upya Marekani.

(AFP)